27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

CRJE yajivunia jengo Taasisi ya Mwalimu Nyerere

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya nchini China, imejivunia miaka 50 ya uwepo wake hapa nchini huku ikiutumia mradi wa ujenzi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation square lililozinduliwa mwishoni mwa wiki na Rais Dk. John Magufuli pamoja na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kama kilele cha uthibitisho wa mafanikio.

Ikiwa ni muelekeo wake mpya katika masuala ya uwekezaji, mradi huo uliojengwa kwa thamani ya Dola za Kimarekani 150 Milioni kutoka Shirika la Kimataifa la kifedha la International Financial Corporation unahusisha uwekezaji wa pamoja baina ya kampuni hiyo ya CRJE na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere.

Wakizungumza wakati wa uzinduzi huo,Marais wote wawili waliipongeza kampuni pamoja na Mfuko wa Mwalimu Julius Nyerere,  kwa mradi huo unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

“Sote tunatambua na kushukuru mapenzi aliyokuwa nayo Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa watanzania na Waafrika katika kupigania usawa, haki na uhuru. Ni wajibu wetu sote kuendeleza jitihada ili kumuenzi kwa vitendo,” alisema Rais Magufuli.

Alisema Watanzania sasa wataweza kujifunza masuala mengi kuhusu Mwalimu Nyerere kupitia taarafa na kumbukumbu muhimu zitakazo patikana katika jengo hilo ikiwemo vitabu, hotuba na vyanzo vingine.

Kwa upande wake Rais Museveni alibainisha kuwa amekuwa mfuasi mkubwa wa Mwalimu Nyerere tangu mwaka 1963 wakati wa jitihada za kutafuta uhuru wa Afrika Mashariki sambamba na jitihada zake katika kukitangaza Kiswahili.

Naye Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke, alisema uzinduzi wa jengo hilo ni kumbukumbu nzuri kwa Hayati Mwalimu Nyerere na uwepo wake unaongeza alama ya uhusiano wa muda mrefu katika ya nchi hizo mbili za Tanzania na China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles