25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kairuki aalika wawekezaji toka China

Tunu Nassor, Dar es salaam

WAZIRI wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angella Kairuki amewaarika wawekezaji kutoka jimbo la Shandong nchini China kuwekeza viwada vya kuongeza thamani nchini kwa kuwa asekta hiyo ina fursa nyingi za ajira nchini.

Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara zaidi 80 waliotembelea nchini mwishoni mwa wiki, Kairuki alisema kuna fursa nyingi za kuwekeza katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Alisema Tanzania imejaaliwa ardhi bora kwa kilimo inayokubali kuzalisha mazao ya chakula na biashara hivyo kuwa na uwezo wa kuzalisha malighafi za kutosha kwa ajili ya viwanda.

“Tumekuwa tukivutia zaidi katika sekta za kilimo na mifugo kutokana na kuajiri watu wengi na tija yake huonekana kirahisi zaidi na ni kubwa kwa taifa,” alisema Kairuki.

Alisema sekta hizo zina mnyororo mkubwa ambao unaweza kuajiri watu wengi ikiwamo katika uzalishaji wa viuatilifu, viuadudu, matrekta, majembe, pembejeo na vifungashio.

 Aisema katika sekta ya uvuvi bado kuna fursa nyingi katika bahari kuu ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa ndio maana wanawaalika wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kushirikiana na wananchi kuwekeza.

Alisema fursa nyingine ni kuwekeza katika viwanda vya utengenezaji wa dawa za binadamu na vifaa tiba.

Aliongeza kuwa kwa sasa Tanzania ina mpango wa kuanza kutengeneza magari hivyo tuna fursa ya kuunganisha magari na kutengeneza vipuri kwa kuwa soko lipo.

“Hapa Tanzania tuna soko la magari la ndani, na Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika na majirani zetu wengine,”  alisema Kairuki.

Naye Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallah Ulega alisema wanawakaribisha kuwekeza mazao ya mifugo na uvuvi hasa katika kusindika.

“Wamekuwa wanunuzi wa mazao ya mifugo na uvuvi hasa ngozi za sangara ambazo wanatengeneza dawa, wananunua mabondo, wananunua ngozi za punda na wamekuja na biashara ya mapembe ya ng’ombe na utumbo,” alisema Ulega.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa biashara wa jimbo la Shandong  Lyu Wei, alisema wanasoko kubwa la kununua magari yaliyotumika.

“Kuna kampuni zaidi 1072 ambazo zinauhusiano na Tanzania kibiashara katika mji wetu ambazo zinazalisha bidhaa mbalimbali zinazoletwa hapa,” alisema Lyu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles