23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Chuo Kikuu Kilimo cha Mwalimu Nyerere Butiama kuanza Oktoba

 MKUU wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo, akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Butiama  na wananchi wanaozunguka  eneo la Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha Mwalimu Julius K. Nyerere, juzi.  Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Lesakit Mellau na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Butiama, Anna Nyamubi.  Picha na Shomari Binda.
MKUU wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo, akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Butiama na wananchi wanaozunguka eneo la Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha Mwalimu Julius K. Nyerere, juzi. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Lesakit Mellau na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Butiama, Anna Nyamubi. Picha na Shomari Binda.

NA SHOMARI BINDA,

KUANZISHWA   Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha Mwalimu Julius K.Nyerere  wilayani Butiama   kutaupandisha na kuuinua mkoa katika masuala mbalimbali  na kuwasaidia wakulima  kuinua kilimo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo,alipotembelea sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya Osward Mang’ombe High School.

Majengo hayo ndiyo  yatakayotumiwa na chuo hicho kinachotarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Oktoba mwaka mwakahuu.

Alisema chuo hicho ambacho kitatoa shahada na stashahada za fani mbalimbali licha ya masuala ya kilimo, kitakuwa chachu kubwa ya maendeleo ya Mkoa wa Mara na wananchi   na kuwataka kujiandaa kukipokea.

Mulongo ambaye alikuwa ameongozana na viongozi wa ngazi ya wilaya, alisema cha kwanza ambacho kinapaswa kuangaliwa ni kuhakikisha migogoro ya aina yoyote baina ya chuo na wananchi haizuki.

Hiyo ni pamoja na  masuala ya ardhi ili  uongozi wa chuo ufanye shughuli zake bila kubughudhiwa.

“Kwanza ni heshima kubwa kuwapo   chuo hiki mkoani Mara na hususan kwenye Wilaya ya Butiama katika kumuenzi mzee wetu Mwalimu   Nyerere na ni muhimu kinapokwenda kuanza kusiwapo na vikwazo vya aina yoyote,” alisema.

Alisema kutokana na taarifa ambazo amepewa na uongozi wa chuo hicho, wananchi wakulima wa kawaida pia watapata fursa ya kupata mafunzo ya muda mfupi  ambayo yatawasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na akawaomba wananchi kujiandaa na hilo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Profesa Lesakit Mellau, alisema   hatua kubwa ya kuanza kwa chuo hicho imekwisha kufikiwa ikiwamo kuanza kuajili wahadhiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles