
NEW YORK, MAREKANI
NYOTA wa timu ya Taifa ya Argentina, Di Maria atakuwa nje ya uwanja katika michuano ya Copa America Centenario, kutokana na kusumbuliwa na nyama za paja.
Mchezaji huyo alipata matatizo hayo katika mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Panama, katika kipindi cha pili cha mchezo huo na nafasi yake ikachukuliwa na Erik Lamela.
Madaktari wamedai kwamba, mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu, hivyo michuano hiyo itakuwa ipo katika hatua za mwisho kumalizika.
Lakini anaweza kucheza katika mchezo wa fainali kama timu yake ya Argentina itafanikiwa kufika hatua hiyo.
Mchezaji huyo alijaribu kufanya mazoezi juzi lakini alishindwa kutokana na maumivu na kujikuta akidondosha chozi huku ikidaiwa kwamba anaililia timu yake ambapo alipanga kuisaidia katika michuano hii.