24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mke wa Vardy apigwa bomu la machozi

Jamie Vardy na mkewe Rebekah Vardy.
Jamie Vardy na mkewe Rebekah Vardy.

MARSEILLE, UFARANSA

MKE wa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England na klabu ya Leicester City, Jamie Vardy, Rebekah Vardy, alikuwa miongoni mwa mashabiki ambao walikumbwa na mabomu ya machozi katika vurugu kati ya England na Urusi baada ya kumalizika kwa mchezo wa Kombe la Euro 2016.

Vurugu hizo zilianza kutokea Ijumaa kabla ya mchezo huo ambao ulipigwa Jumamosi, inadaiwa kwamba chanzo cha vurugu ni mashabiki wa England kukesha kunywa pombe kali kwa ajili ya kusubiri mchezo wao, hivyo wakaanza kuwavamia wapinzani wao Urusi.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki walikamatwa na polisi kutokana na vurugu hizo, lakini baada ya kumalizika kwa mchezo ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1, mashabiki hao walianzisha tena vurugu ndani ya uwanja ndipo polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kwa ajili ya kutuliza gasia.

Katika mashabiki ambao waliguswa na moshi wa mabomu hayo ni mke wa Vardy, kutokana na eneo ambalo alikaa ndipo vurugu zilipoanzia.

“Nimeona kwa macho yangu vurugu zikianza, ukweli ni kwamba hakuna ubinadamu ambao ulifanyika kwa kuwa watu wameumizana vibaya bila sababu za msingi.

“Niliteseka na mabomu ya machozi kwa kuwa yalinipata, lakini nashukuru kuwa salama,” alisema Rebekah. Vardy amefunga ndoa na mrembo huyo siku chache kabla ya michuano hiyo ya Euro kuanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles