23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Xhaka aipa familia asilimia 80 ya mshahara

Granit Xhaka
Granit Xhaka

MARSEILLE, UFARANSA

NYOTA mpya wa klabu ya Arsenal na timu ya Taifa ya Switzerland, Grant Xhaka, ameweka wazi kwamba anaipa familia yake asilimia 80 ya mshahara wake.

Mchezaji huyo ambaye amesajiliwa na klabu ya Arsenal Mei mwaka huu kwa kitita cha pauni milioni 33.1, akitokea klabu ya Borussia Monchengladbach, amedai familia yake ndiyo kila kitu kwake.

“Nadhani bado nina deni kwa wazazi wangu kwa kuwa walinipa kila kitu hadi nafika hapa, sasa huu ni wakati wao wa kula matunda yangu.

“Kutokana na hali hiyo, ninaona bora nitoe asilimia 80 ya mshahara wangu kutoka kwenye soka kila mwezi kwa ajili ya familia nyumbani.

“Mimi ni kijana nina uwezo wa kutafuta fedha kwa sasa, hivyo ni vizuri nikawa naisaidia familia yangu ambayo imenifikisha hapa ili nizidi kupata baraka. Unaweza ukawa na fedha nyingi kwenye akaunti yako lakini ikawa haina maana yoyote kama utashindwa kuzifurahia ukiwa na familia yako.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles