26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl Nyerere chajivunia bunifu za wanafunzi wake

Na Rose Itono, Dar es Salaam

Uongozi wa Chuo cha Kumbhkumbu ya Mwalimu Nyerere umesema miradi ya ubunifu iliyobuniwa na wanafunzi wake itasaidia kutatua changamoto mbalimbaki zinazoikabili jamii

Akizungumza kwenye maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam jana Mratibu wa mafunzo ya Shahada za Awali chuoni hapo Dk. Samwel Lunyelele alisema chuo kinajivunia bunifu mbalimbal za wanafunzi wake ikiwepo ya malipo ya maji kabla ya kutumia

Dk. Lunyelele alisema chuo kimezalisha wabunifu mbakimbali ambao watasaidua kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.

Akizungumzia ubunifu wake Jumbe Kambaya ambaye ni mwanafunzi wa chuo hicho aliyebuni
mita ya maji ya malipo kabla alisema mita hiyo itamuwezesha mtumiaji kulipia maji kupitia mitandao ya simu kabla ya kutumia na kisha atapokea namba (token) kutoka kampuni husika na kisha kuingiza namba aluzotumiwa katika mita yake kwa kutuma ujumbe kwenye namba ya mita yake

Aliongeza kuwa utumiaji wa njia hiyo utapunguza malalamiko ya Wareham juu ya usomaji wa mita

Naye Peter Mwakalesya mwanafunzi mwingine wa chuo hicho aliyebuni ubao unaofuta wenyewe. Alisema ubao huo utatatua tatizo la walimu kutumia nguvu nyingi na kuwapunguzia muda

“Walimu wanatumia nguvu nyingi katika kufuta ubao na kupoteza Musa mwingi, “alisema Mwakalesya

Aluzitaja faida za ubao huo kuwa mbali na kupunguza muda pia zitawapunguzia walimu aza mbalimbali za kiafya wanazokutana Nazi walimu kwa ufutaji ubao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles