30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

DIT yawataka Watanzania kuwa na utamaduni wa kununua bidhaa za ndani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imewataka Watanzania kuwa na Utamaduni wa kununua bidhaa za ndani ili Uchumi wa Viwanda uweze kukua zaidi.

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimatafa (DITF) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,(DIT) Profesa Preksedis Ndomba amesema bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa zikidhalishwa chini zipo katika Viwango hivyo ni muhimu watanzania kuziamini .

Ndomba amesema kazi kubwa ya DIT ni kuchachua maendeleo ya viwanda nchini ndio maana wamejikita zaidi katika teknolojia za kisasa.

Amesema licha ya kuwa na teknolojia za kisasa taasisi yao inapokea na kuendelrza bunifu mbalimbali za wadau.

“Bidhaa zinazotengenezwa Tanzania ni imara na nzuri kwa ajili ya matumizi hivyo watanzania wawe na utamaduni wa kununua na kutumia bidhaa za ndani,” alisema Prof. Ndomba.

Kwa upande wake Mkuu wa Mahusiano na Viwanda DIT John Msumba alisema,katika maonyesho ya mwaka huu wamekuja na product mpya kwa ajili ya kutengeneza vipuli.

Dk.Msumba amesema DIT imejipambanua katika shughuli zake kwa ajili ya kuleta tija katika hasa kwenye uchumi wa viwanda.

Naye Ofisa Uhusiano Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT)Regina Kumba amesema DIT ni kampuni inayotoa nafasi kwa vijana kuwawezesha kufanya kazi kwa vitendo.

Amesema hivi sasa tayari wameshawawezeha vijana wengi ambao tayari wameshaanza shughuli mbalimbali za kujiajiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles