Chris Brown akamatwa kwa udhalilishaji

Chris Brown
Chris Brown

LOS VEGAS, MAREKANI

POLISI nchini Marekani, wamemkamata nyota wa muziki wa RnB nchini humo, Chris Brown, kwa tuhuma za kumshambulia msichana ndani ya nyumba yake.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana, ambapo mwanamke huyo mwanamitindo, Baylee Curran, alidai kwamba aliitwa na msanii huyo kwa ajili ya mambo ya kibiashara, lakini alishangaa kuona msanii huyo akimtolea bunduki na kumtisha.

Polisi waliwasili kwenye nyumba ya msanii huyo saa tisa usiku na kumkamata, Chris Brown, huku akisubiria kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hata hivyo, kupitia akaunti yake ya Instagram, msanii huyo ameonekana kuwatupia lawama polisi hao kwa kumsumbua usiku huo wa manane. Kipindi cha hivi karibuni msanii huyo amekuwa akituhumiwa kuhusika katika matukio mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here