Christian Bella kunogesha Miss Kinondoni kesho

Christian Bella
Christian Bella
Christian Bella

Na ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

MWANAMUZIKI Christian Bella, anatarajia kutumbuiza kesho kwenye shindano la kumsaka Miss Kinondoni linalotarajiwa kufanyika Ukumbi wa Defrance, Sinza jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwakutanisha warembo hao na wadhamini wa shindano hilo kinywaji cha Windhoek, Ofisa mauzo wa kampuni hiyo, Andrea Misama, alisema kwa mwaka huu warembo wengi walijitokeza tofauti na miaka ya nyuma.

“Tunawapongeza wazazi kwa kutambua faida ya mashindano ya urembo kwa kuwaruhusu kwa wingi watoto wao kushiriki katika mashindano haya tofauti na mwaka jana na sisi hatutawaangusha tunaahidi kutekeleza malengo yetu ya kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao,” alieleza.

Kwa upande wao warembo watakaoshiriki shindano hilo wameahidi kuonyesha vipaji vyao huku wakiomba wadau na mashabiki wa urembo wajitokeze kwa wingi siku ya shindano ili waweze kuburudika na pia kuona wawakilishi wao katika mashindano ya Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here