30.4 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

CHINA: AFRIKA IWE NA SAUTI UN

Msemaji wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga
Msemaji wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga

NA MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM


CHINA imeanza kufanya kampeni ya kuzihamasisha nchi za Afrika ziweze kudai mageuzi ndani ya  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN).

Nchi hiyo, imeweka wazi kuwa inaunga mkono msimamo wa Afrika na Tanzania wa kutaka bara hilo lipewe viti viwili vya kudumu kwenye baraza hilo na kura ya turufu.

Mbali na hayo, China inatarajia kuwekeza kwa kujenga viwanda takribani 200 nchini kabla ya mwaka 2020.

Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Msemaji wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga wakati akizungumzia ujio wa  ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ambaye atawasili nchini  wiki ijayo.

Alisema Yi atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania kuhusu uwekezaji wa viwanda vidogo  na kati.

Kasiga alisema China iliichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nne barani Afrika, zitakazowezeshwa kupiga hatua kwenye maendeleo ya viwanda.

“Mategemeo ya uwekezaji wa viwanda hivi,utazalisha ajira zaidi ya 200,000 na ndiyo maana tulichagua viwanda ambavyo vitatumia raslimali watu zaidi kuliko mashine na vitakuwa viwanda vya kiwango cha kati na vidogo,” alisema Kasiga.

“Katika ziara hii, Yi atakutana na Rais Dk.John Magufuli na kuzungumzia miradi mingine ya miundombinu ikiwa ni pamoja na maboresho makubwa ya reli ya TAZARA, ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na reli ya kati.

“Katika ziara hiyo, Yi atapokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahinga, akiwa na wajumbe 10 atakaoongozana nao pamoja na waandishi wa habari kutoka China,” alisema Kasiga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles