25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI MTWARA WAKAMATA SHEHENA YA KOROSHO

korosho-1024x650

NA FLORENCE SANAWA, MTWARA  


 

MAMLAKA ya Bandari Mkoa wa Mtwara, wamelazimika kuzuia magari mawili yenye magunia ya korosho 350 sawa na tani 29, baada ya kubainika mihuri iliyotumika kwenye vibali ni ya kughushi.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara, Mhandisi Juma Kisaura alisema mzigo huo ulitiliwa shaka hali ambayo ililazimu askari wa bandari hiyo kuomba vibali ambavyo pia vilitiwa shaka.

Alisema mzigo huo, uliokuwa umepelekwa bandarini hapo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi, ulisimama kwa muda ili  taratibu za ndani ya Bandari zifanyike.

“Hata tulipowaita wenzetu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ili wafanye ukaguzi walikana hawaitambui mihuri hiyo…  kwa kuwa mamlaka ina askari wake na hawana mamlaka ya kuchukua hatua zaidi ya hapo, tumeikabidhi jeshi la polisi kuendelea na hatua zingine za kisheria,” alisema Kisaura.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Halima Dendego aliyefika bandarini hapo, alisema wafanyabiashara wanatakiwa kuwa makini kwa kuwa mkoa huo umejipanga vizuri kukomesha uuzwaji wa korosho kwa njia haramu.

Alisema upo mpango kabambe wa kuhakikisha wakulima wa korosho,wanapata stahiki zao vizuri bila kuwaruhusu wafanyabiashara wajanja wajanja kuwarubuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles