22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

CHENGE SASA NI ‘BWANA RELI’

Gabriel Mushi, Dodoma

Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge ameendelea kuzua gumzo kutokana na majina aliyojipachika baada ya kuwataka wabunge wamuite ‘bwana reli’,

Chenge ametoa kauli hiyo bungeni leo Mei 10, jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

“Mimi kuanzia leo mniite bwana reli. Niiteni jina langu hilo kuanzia leo. Kwa sababu nitakuwa nachangia kwa kila wizara hata kama sitahusika nayo.

“Mimi nimshukuru Rais kwa uamuzi wake na tutaona tukapokamilisha reli hii, uchumi wa Tanzania utaibuka kama uyoga, ikumbukeni tarehe ya leo, bwana reli asema,” amesema Chenge.

Pamoja na mambo mengine akichangia mjadala wa wizara hiyo Chenge amesema bado anasumbuliwa na suala zima la gharama za uwekezaji nchini.

“Bado zipo juu sana, naona kwenye hotuba hii hali ya upatikanaji wa umeme, maji na miundombinu mingine yote bado inasuasua wakati inapaswa gharama zishuke,” amesema.

Mwaka 2008, Chenge alipachikwa jina la ‘mzee wa vijisenti’ baada ya kudaiwa kuwa na fedha ambazo zilikuwa ni zaidi ya Dola za Marekani milioni 40 katika kashfa ya rada zilikuwa sawa na vijisenti.

Aidha, mwaka 2009 Chenge alitawazwa kuwa mtemi wa kabila la Wasukuma-Bagole, Kanda ya Itilima, wilayani Bariadi hivyo kupachikwa jina la ‘Mtemi Chenge’ ambalo amekuwa akilitumia hadi sasa katika vikao mbalimbali vya Bunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,169FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles