29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

KOMU: SERIKALI INAHAMISHA GOLI MIRADI YA LIGANGA, MCHUCHUMA

Gabriel Mushi, Dodoma

Waziri Kivuli wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Anthony Komu amesema sera ya viwanda imeipa kisogo miradi ya Liganga na Mchuchuma jambo linaloilazimu Serikali kuagiza chuma nje ya kwa ajili ya ujenzi wa reli na malighafi za viwanda vya nondo nchini.

Akichangia mjadala wa bajeti ya viwanda, biashara na uwekezajio, Komu amesema licha ya miradi hiyo kuanza kuzungumziwa miaka kadhaa iliyopita, serikali imeendelea kupiga danadana kuitekeleza.

Komu ambaye pia ni Mbunge wa Moshi vijijini (Chadema), amesema mwenendo huo unadhihirisha kuwa uwekezaji unaofanywa kwenye sekta ya viwanda hauwezi kuonesha dalili njema iwapo hakutakuwapo na maji ya kutosha.

“Sasa miradi ya gesi asili haijatumika vya kutosha lakini cha ajabu serikali imekimbilia kuwekeza kwenye Stiggler’s Gorge na kuanzisha vita na mataifa mengine duniani, ambayo ni sawa na kuhamisha goli, hapakuwa na ulazima huo hasa ikizingatiwa miradi mikubwa iliyoanzishwa haijatumika ipasavyo wala kutengamaa,” amesema.

Amesema miradi ya gesi asilia imetumika kwa asilimia 10 pekee huku miradi ya Liganga, Mchuchuma na Engaruka ikitelekezwa.

“Kila siku serikali inajitetea kwa kuhamisha goli sasa na kukimbilia kwenye Stigglers Gorge, sijui Magufuli nayeye anataka kuwa na mradi wake? Amehoji.

Aidha, ameitaka Serikali kuangalia namna bora ya kufufua mashine ambazo zipo katika viwanda mbalimbali nchini kwa kuwa nyingi zimechakaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles