27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Chameleone apokelewa kama rais Congo

ChameleoneKINSHASA, CONGO

NYOTA wa muziki nchini Uganda, Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’, amezidi kung’aa nchini Congo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya mapokezi yake kufananishwa na ya rais.

Msanii huyo ambaye anafanya vizuri zaidi ya miaka 16 nchini Uganda, aliwashangaza mashabiki nchini Congo baada ya kuwasili kwa ajili ya onyesho lake, ambapo kwenye uwanja wa ndege alipokelewa na wanajeshi na polisi kama ilivyo katika mapokezi ya rais hivyo kuwashangaza wasanii wakubwa nchini humo.

Hata hivyo, baada ya kumaliza shoo hiyo, Chameleone kupitia akaunti yake ya Instagram aliwashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika onyesho hilo.

“Mimi ni mtu wa watu, hauwezi kunipata katika makundi ya watu, lakini utanipata katika mioyo yao, asante kwa watu wote wanaonipenda na kuungana na mimi, nawapenda sana watu wangu wa Congo,” aliandika Chameleone.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles