23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Johari: Sitaki filamu za mazoea

JOHARINA JANETH MAPUNDA (MSPS)

NYOTA wa filamu nchini, Blandina Chagula ‘Johari’, amesema anajipanga ili akitoa filamu ziwe nzuri zitakazoendana na matakwa ya mashabiki wake.

Johari alisema ukimya wake haumaanishi kuishiwa kisanaa bali ni mbinu anayoitumia kutafakari ili akirudi awe mpya kwa mashabiki na kwenye kiwanda cha filamu kwa ujumla.

“Unajua usifanye kazi kwa mazoea ili uonekane, unatakiwa kufanya kazi zenye hadhi na zikonge nyoyo za Watanzania ndiyo maana nipo kimya kwa muda ili nikirudi kila mmoja ajue nimerudi kweli kwa mabadiliko ya kisanaa na si kurudi kwa mazoea,” alieleza Johari.

Aliongeza kwa kuwaomba Watanzania wawe wazalendo wa kuunga mkono kazi za wasanii wao kwa kununua nakala halisi huku akijigamba kwamba ujio wake mpya wa filamu anayoiita ‘True love never die’ aliyocheza na nyota Richie, Irene Uwoya na wasanii wengine kibao itaendelea kubamba sokoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles