19.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Shoo ya Koffi yaamsha mori za bendi nchini

DSC_2951NA MWANDISHI WETU

SHOO ya mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi barani Afrika kutoka Congo (DRC), Koffi Olomide ‘Mopao Mokonzi’ iliyofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Escape One Mikocheni, imeongeza hamasa kwa bendi za muziki wa dansi nchini kujifunza namna ya kudumu kwa muda mrefu katika muziki huo huku ukiwa katika ubora wako.

Katika onyesho hilo lililokuwa na shamra shamra za kupiga ‘selfie’ kwa idadi kubwa ya mashabiki waliofurika katika ukumbi huo, wanamuziki wa bendi walionyesha ukomavu na moyo wa kufanya zaidi ya anavyovifanya Koffi katika video na maonyesho yake mbalimbali waliyoshuhudia.

Kiongozi wa kundi la Malaika Bendi, Christian Bella, Bendi ya Mapacha watatu, Ruby na wasanii mbalimbali walionyesha namna walivyoguswa na umaarufu wa muda mfupi wa wimbo wa ‘selfie’ wa Koffi huku wakionekana kuimba kwa kujiamini katika onyesho hilo.

Koffi na kundi lake la Quartier Latin, lilijaa wanenguaji wenye vipaji na upeo wa kutambua namna ya kuwateka mashabiki kiasi cha kutaka waendelee kuimba kila walipomaliza wimbo.

Walipokuwa jukwaani kundi hilo lilionyesha ukomavu wa muda mrefu katika muziki wa dansi kwa kutumbuiza nyimbo za albamu zao tofauti wakichanganya za zamani na nyimbo mpya kiasi kwamba mashabiki walisuuzika nyoyo zao ipasavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles