Ne-Yo awanyanyua Ali Kiba, Vanessa Mdee, Ben Pol, Fid Q

0
1394

Neyo na Ali kibaNA MWANDISHI WETU

MWIMBAJI maarufu duniani wa miondoko ya R&B kutoka Marekani, Ne-Yo, ameacha gumzo kwa wapenzi wa muziki wanaofuatilia onyesho la Coke Studio kutokana na umahiri aliouonyesha katika kolabo alizofanya na wasanii kutoka barani Afrika.

Katika msimu huu, amefanya kolabo na wanamuziki Wangechi (Kenya), Ali Kiba (Tanzania), Maurice Kirya (Uganda), Dama Do Bling (Msumbiji) na  Ice Prince (Nigeria).

Kolabo alizofanya na wasanii hao zimeleta burudani ya pekee kwa wapenzi wa muziki wa onyesho hilo linaloleta msisimko wa aina yake kwa mashabiki.

Mwanamuziki huyo ambaye ni msanii mwalikwa kwenye msimu huu, anatamba na vibao vyake vikiwa ni ‘Let Me Love You’, ‘Beautiful Monster’, ‘Coming With You’ na  ‘She Knows’ aliomshirikisha Juicy J.

Kampuni ya Coca-Cola kwa mara nyingine kupitia kampeni yake ya ‘Sababu Bilioni za Kuamini’, inaendelea kuleta onyesho hilo msimu wa tatu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here