27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga sc kamili yaifuata Mgambo Tanga

YangaNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya Yanga kinatarajiwa kuelekea jijini Tanga leo, tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mgambo Shooting uliopangwa kufanyika Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani humo.

Kwa mujibu wa kocha mkuu wa Yanga, Hans Van der Pluijm, ataondoka na wachezaji wote wa timu hiyo na anatarajia kupanga kikosi kitakachoshuka dimbani kesho jioni.

Pluijm alisema kuwa awali walikuwa na mpango wakuweka kambi mjini Bagamoyo, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao waliamua kuahirisha zoezi hilo.

“Kambi ya Bagamoyo ilikuwa ni mkakati wetu wa kwanza kujiwinda na mchezo dhidi ya Mgambo, lakini zipo sababu muhimu zilizopelekea tuahirishe, sasa tutawafuata wapinzani wetu bila kuweka kambi yoyote,” alisema.

Mholanzi huyo alieleza wanaelekea jijini Tanga, wakiwa na lengo la kuchukua pointi tatu muhimu na kukiwezesha kikosi hicho kuendeleza gurudumu la ushindani waliloanza nalo msimu huu.

“Maandalizi tuliyofanya yanatosha kuwafunga Mgambo, ndiyo maana hata kama tumeshindwa kuweka kambi kama tulivyokuwa tumepanga mwanzo, bado tuna matumaini ya kushinda mchezo huo,” alisema Pluijm.

Timu hiyo inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na jumla ya pointi 23 kutokana na michezo tisa iliyocheza sawa na Azam FC inayoongoza ligi hiyo kwa pointi 25.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles