29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Celine kufanya onyesho la mwisho na mumewe

Celine DionLOS ANGELES, MAREKANI

MKALI wa sauti, Celine Dion, amesema kuwa anatarajia kufanya shoo ya mwisho siku ya Krismasi akiwa na mume wake, Rene Angelil.

Celine amekuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kumuuguza mume wake huyo ambaye anasumbuliwa na kansa. Hivi karibuni msanii huyo alikuwa akizunguka na mume wake katika maonyesho yake mbalimbali.

Lakini msanii huyo amesema kuwa siku ya sikukuu itakuwa mwisho kufanya shoo akiwa na mume wake, kwa kuwa hali yake haitamwezesha kuzunguka naye kama anavyofanya sasa.

“Hali ya mume wangu kwa sasa inaendelea vizuri, lakini natarajia kufanya shoo ya mwisho nikiwa naye siku ya Krismasi mwaka huu, baada ya hapo nitamuacha nyumbani apumzike,” alisema Celine.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles