25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yampa tano Rais Samia kwa kunyanyua sekta ya elimu

Na Mwandihi Wetu, Mtanzania Digital

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinaridhishwa na utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Elimu, ambapo bajeti ya Wizara hiyo imeongezeka kutoka Sh Bilioni 464 hadi Sh bilioni 570.

Katika kuhakikisha elimu inaboreshwa, CCM imesema Serikali imetoa msamaha wa Sh trilioni 1.1 kwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Akizungumza wakati alipotembelea maonesho ya 17 ya vyuo vikuu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu ameipongeza na kuishukuru serikali kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu.

“Kama chama tumefika kuona serikali tuliyoipa madaraka inavyotekeleza ilani, nimeona maboresho makubwa na utoaji wa huduma za moja kwa moja, imeondoa urasimu kwa kiasi kikubwa wa wahitaji kufika eneo la huduma,” amesema Shaka.

Shaka amesema kuwa kufuatia maboresho katika sekta hiyo, udahili umeongezeka kutoka 87,934 kwa mwaka huu hadi 106,020.

“Ukitaka kuona mabadiliko yamefanyika tumeambiwa ongezeko la wahitimu liomeongezeka halikuja bure bure ni kwa sababu mazingira rafiki yametengenezwa kwa vijana wanufaika, aliyetengeneza ni Rais katika wote mnafahamu kuwa ametengeneza mazingira rafiki,” amesema Shaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles