24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia apongezwa kwa kuimarisha miundombinu Rukwa

*Bilioni 2.5 zakamilisha ujenzi wa daraja la Kisalala

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kazi anayoifanya kuboresha miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Rukwa ikiwemo kukamilika kwa daraja la Kisalala lenye urefu wa mita 35 katika barabara ya Laela kwenda Mwimbi hadi Kizombwe lililogharimu Sh bilioni 2.5.

Pongezi hizo zimetolewa Julai 21, 2022 na wananchi wa kitongoji cha Tiswe mji mdogo wa Laela wilaya ya Sumbawanga mkoa wa Rukwa kupitia Mwenyekiti wao Frolence Uliza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Geofrey Kasekenya.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa daraja la Kisalala umekuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi wa vijiji vya Kisalala na Mwimbi kuweza kuvuka bila shida.

Nae, Elizabeth Kalungwizi mkazi wa kijiji cha Kisalala alisema anaishukuru Serikali kwa kutatua changamoto ya uvukaji kwenye daraja hilo kwani ilikuwa ngumu kipindi cha mvua lakini sasa wanapita vizuri darajani hapo.

Akizungumza kwenye ziara hiyo Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Kasekenya alisema Rais Samia Suluhu Hassan amekusidia kuifungua nchi kupitia miundombinu ya kisasa kwa kuwa anatambua uchumi utastawi kupitia uwepo wa barabara bora na za kisasa.

“Hii barabara ya Laela kupitia Mwimbi hadi Kizombwe katika wilaya ya Sumbawanga inafika Matai hadi bandari ya Kasanga iliyopo Ziwa Tanganyika hivyo magari makubwa ya mizigo yatafikisha bidhaa kwenda katika soko la nchi ya Kidemokrasia ya Kongo,” alisisitiza Mhandisi Kasekenya.

Mhandisi Kasekenya aliwapongeza wataalam wa TANROAD kwa kusanifu daraja hilo na kusimamia ujenzi wake uliofanywa na mkandarasi mzawa M/s Mselem Civil Engineering and Contractors wa Sumbawanga.

Naibu Waziri huyo baada ya kukagua daraja hilo alitoa agizo kwa Wakala wa Barabara mkoa wa Rukwa (TANROAD) kuhakikisha kuwa kabla ya Agosti 23, mwaka huu kazi hiyo iwe imekamilika kwa mujibu wa mkataba na kuwa mkandarasi asimimiwe kikamilifu kumaliza kazi hiyo kwa ubora ulikusidiwa.

Meneja wa TANROAD Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo wa daraja la Kisalala ulianza Oktoba, 2021 na utamilika Agosti 7 mwaka huu ambapo umegharimu Sh bilioni 2.5 na kuwa tayari sasa magari yanapita na kazi iliyobaki ni ujenzi wa kingo za mto.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya M/s Mselem Civil Engineering, Mselem Nassor alisema kazi imekamilika kwa asilimia 99 na kuwa amepokea malekezo ya Serikali kupitia Naibu Waziri kukamilisha mradi huo kwa ubora.

Mselem alitoa ombi kwa Serikali kuendelea kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wazawa ili waweze kushiriki kujenga uchumi wa nchi kupitia kazi za ujenzi wa miradi kwa kuwa wana wataalam na vifaa vya kisasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles