25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Casillas: Nakaribia kustaafu soka

Iker CasillasMADRID, HISPANIA

MLINDA mlango wa zamani wa klabu ya Real Madrid, Iker Casillas, amedai kwamba wakati wake wa kustaafu soka la timu ya Taifa unakaribia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye anakipiga katika klabu ya Porto ya nchini Ureno, amesema amekuwa na furaha kubwa kuitumikia timu yake ya Taifa ya Hispania kwa kucheza michezo 166, hivyo ni wakati wa kuwapa nafasi wachezaji wengine.

“Katika kipindi cha miaka ya karibuni nilikuwa na wakati mgumu na kuna wakati nilikuwa vizuri, lakini ninaamini nitaendelea kuwa katika ubora wangu.

“Naweza kusema kwamba wakati wangu wa kustaafu soka unakaribia sana hivyo nitakuja kuweka wazi kwamba ni lini nitaachana na soka la timu ya Taifa.

“Lakini ninaamini nitakuja kuwa karibu na timu ya vijana kwa ajili ya kutoa mchango wangu, lakini sina uhakika kama huu utakuwa ni mwaka wangu wa mwisho na timu ya Taifa ya Hispania.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles