24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Curry awatuliza mashabiki Warriors

Stephen CurryNEW YORK MAREKANI

NYOTA wa mchezo wa kikapu wa timu ya Golden State Warriors, Stephen Curry, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo ambao walishtushwa na majeruhi yake.

Mchezaji huyo alipata majeruhi mwishoni mwa wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Oklahoma City, huku Warriors ikishinda vikapu 121-118.

Katika mchezo huo, Curry alipatwa na maumivu ya kifundo cha mguu na kuwapa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo kutokana na mchango mkubwa wa mchezaji huyo.

“Nashukuru Mungu ninaendelea vizuri japokuwa nilipatwa na maumivu makali, lakini kwa sasa nipo vizuri kwa kucheza.

“Nilitumiwa ujumbe mbalimbali kutoka kwa mashabiki wangu na wadau wa kikapu, ila niwatoe wasiwasi kwamba nipo vizuri kwa sasa,” alisema Curry.

Nyota huyo ametoa mchango mkubwa katika kikosi hicho msimu huu na kukifanya kishinde michezo 53 kati ya 58 waliyocheza, huku msimu uliopita akiwa mchezaji bora wa MVP.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles