27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldo amwandaa mwanawe kuwa mchezaji bora

Cristiano JrMADRID, HISPANIA

NYOTA wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amesema anamwandaa mtoto wake, Cristiano Jr, kuja kuwa mchezaji bora duniani kama alivyo yeye.

Cristiano Jr ambaye ana umri wa miaka mitano, tayari ameanza kuonesha dalili ya kuja kuwa mchezaji mzuri wa soka kutokana na mazoezi ambayo anapewa na baba yake, hivyo Ronaldo anaamini mtoto huyo ataweza kufuata nyayo zake.

“Nahitaji mwanangu aje kuwa mchezaji bora wa soka duniani, mimi mwenyewe ni mchezaji mkubwa na mtoto wangu nataka aje kuwa hivyo.

“Nadhani ana kitu fulani tofauti ambacho anaweza kuja kushangaza dunia kwa kuwa ana tabia ya uanamichezo, kwanza bado mdogo na anapenda sana soka,”  alisema Ronaldo alipofanya mazungumzo na kituo cha runinga cha Zhejiang Satellite TV cha nchini China.

Hata hivyo, Ronaldo amesema kwamba hawezi kumlazimisha mwanawe kuja kuwa mchezaji, akikua ataamua kufanya kile ambacho atakipenda mwenyewe.

“Ndani ya nyumba yangu kuna mipira 30, muda mwingi anatumia kuichezea, hivyo ninaamini atakuja kuwa mchezaji na napenda aje kuwa kama mimi katika maisha yake,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles