31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Ibrahimovic aweka wazi kuitaka Ligi Kuu England

IbrahimovicPARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya PSG, Zlatan Ibrahimovic, ameweka wazi kwamba atajiunga na klabu ya Ligi Kuu nchini England msimu ujao.

Nyota huyo ambaye anawaniwa na timu kubwa nchini England kama vile Manchester City, Manchester United, Arsenal na Chelsea, mchezaji huyo amedai kwamba hana sababu ya kuendelea kuwa PSG msimu ujao.

Hata hivyo, mchezaji huyo mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo amedai hadi sasa hajafanya mazungumzo yoyote na klabu yake juu ya mkataba mpya.

“Ni kweli klabu kubwa nchini England zinanihitaji, ninaamini ligi yao ina jina kubwa duniani na wachezaji wengi wanavutiwa kucheza ligi hiyo.

“Lakini kwa upande wangu nasubiri kuona klabu ambayo itaweka fedha mezani na kukubaliana na ndipo nitafanya maamuzi. Hii ni kama ndoa lazima pande zote mbili ziwe na furaha.

“Ila kwa sasa bado nina mkataba na klabu yangu hadi mwishoni mwa Juni, lakini baada ya kumaliza mkataba huo siwezi kuendelea kuwa PSG.

“Mambo mengi tutayaona wakati wa majira ya joto, lakini kwa upande wangu ninaamini mambo yatakuwa mazuri,” alisema Ibrahimovic.

Mchezaji huyo kwa sasa ana jumla ya mabao 35 kati ya michezo 40 aliyocheza msimu huu akiwa na klabu hiyo na kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles