29.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ndoa ya Mariah Carey yaahirishwa

mariah-carey na james-packerNEW YORK, MAREKANI

NDOA ya msanii maarufu wa muziki duniani, Mariah Carey na tajiri wa nchini Australia, James Packer, imeahirishwa kutokana na ratiba ya muziki ya msanii huyo kumbana.

Wawili hao walipanga kufunga ndoa hivi karibuni lakini kutokana na msanii huyo kubanwa na ratiba ya muziki itakayomfanya atumie muda mwingi kuzunguka kwa ajili ya shoo, ameona bora waahirishe hadi watakapoipanga upya.

Awali walisema watafunga ndoa mapema iwezekanavyo mara baada ya tajiri huyo kumvisha pete Mariah yenye thamani ya dola milioni 7.

“Kila kitu kina mipango yake, tulipanga kufunga ndoa mapema mwaka huu lakini mambo yamekuja kuingiliana hivyo itakuwa ngumu, ila kila kitu kitakuwa sawa baada ya kumaliza ratiba yangu ya muziki, samahani kwa usumbufu,” aliandika Mariah kwenye akaunti yake ya Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles