24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

T.I afikisha watoto saba

T.I na Mke wakeNEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki nchini Marekani, Clifford Harris ‘T.I’, amefanikiwa kupata mtoto wa kike kutoka kwa mke wake wa sasa, Tameka Tiny.

Msanii huyo kwa sasa amefikisha jumla ya watoto saba, huku mke wa sasa akiwa amezaa naye watoto watatu na wengine wakizaliwa na mama tofauti.

Kupitia akaunti yake ya Facebook, msanii huyo ameandika kwamba amekuwa na furaha kubwa katika sikukuu ya Pasaka baada ya kuongeza ukubwa wa familia yake.

“Pasaka imekuwa nzuri kwangu kwa kuwa tumefanikiwa kumpokea mgeni wetu mpya, tunashukuru sana kufanikiwa kumpata mtoto wa kike na sasa familia inazidi kukua. Nampongeza mama watoto wangu kwa kujifungua salama ninaamini ana furaha kubwa,” aliandika T.I.

T.I mwenye umri wa miaka 35, amekuwa kati ya wasanii wenye watoto wengi akiwa na umri wa miaka 45, lakini amezidiwa na DMX mwenye watoto 12.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles