23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

CAG AOMBA RADHI KUSEMA DENI LA TAIFA NI ASILIMIA 72


Na SARAH MOSES-DODOMA    |

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, ameomba radhi kwa maelezo aliyotoa wakati wa kuwasilisha ripoti ya mwaka ya ukaguzi kwa Rais Dk. John Magufuli.

Katika hafla hiyo iliyofanyika wiki hii Ikulu, Dar es Salaam, Profesa Assad alisema deni la taifa ni asilimia 72 na kwamba usahihi wa deni hilo ni asilimia 71.

“Taarifa zangu zote zilizoandikwa kwa maandishi, hazina tatizo ila nilichokiongea mdomoni ndicho hakikuwa sahihi, hivyo naomba radhi kwa wananchi na Serikali kwa usumbufu uliojitokeza,” alisema Assad.

Alisema taarifa sahihi kuhusu mwenendo wa deni la Taifa kwa mujibu wa taarifa ya maandishi iliyowasilishwa kwa Rais inaonyesha hadi kufikia Juni 30 mwaka 2017, deni lilikuwa Sh trilioni 46.08.

“Kati ya deni hilo, deni la ndani ni Sh trilioni 13.34 ambapo nia sawa na asilimia 29, na deni la nje ni Sh trilioni 32.75 sawa na asilimia 71.

“Hivyo basi deni la nje ni asilimia 31 ya pato la Taifa (GDP), pia ukaguzi umebaini kuwa deni la taifa kwa sasa ni himilivu,” alisema.

Aidha Profesa Assad alisema licha ya tukio la kukabidhi ripoti hiyo kurushwa mubashara na Kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC), bado ripoti za CAG za ukaguzi wa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2017 zitabaki kuwa za …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles