29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

BUNGE LA BRAZIL LAMWOKOA RAIS TEMER

BRASILIA, BRAZIL

BUNGE la Brazil limepiga kura kupinga mashtaka ya rushwa dhidi ya Rais Michel Temer na hivyo kumuepusha kufikishwa mahakamani, hatua ambayo pia ingesababisha aondolewe madarakani.

Wabunge wa Brazil wameyatupilia mbali mashtaka ya rushwa yaliyokuwa yanamkabili rais huyo anayeelemewa na kashfa na hivyo kumuepusha na kuwa rais wa pili wa Brazil kuondolewa madarakani katika kipindi cha mwaka mmoja.

Licha ya kukabiliwa na madai mazito ya kupokea hongo, Temer alitarajiwa kuponyoka na kuendelea kuwa madarakani.

Hata jinsi alivyoponyoka kirahisi ni jambo la kushangaza kipindi, ambacho Brazil iko katika kampeni kubwa ya kupambana na rushwa.

Bunge la chini lilihitaji wingi wa theluthi mbili ya kura kuruhusu afunguliwe kesi Mahakama Kuu.

Hata hivyo Rais Temer alihitaji kupata thuluthi moja tu ya wabunge ili kumuunga mkono au kutopiga kura ili mashtaka yaliyokuwa yanamkabili yatupiliwe mbali.

Temer hatimaye aliungwa mkono na wabunge 263 kati ya 513.

Rais huyo wa Brazil ameyaita matokeo hayo kuwa ushindi wa wazi na kwamba haukuwa wake bali demokrasia katika nchi inayofuata utawala wa sheria.

Kiongozi huyo wa Brazil ameeleza kwamba kutokana na uamuzi huo ulio wazi sasa anaweza kusonga mbele katika kuchukua hatua za lazima ili kuitimiza kazi ambayo serikali yake iliianzisaha mwaka mmoja uliopita.

Iwapo bunge la Brazil lingeruhusu kesi hiyo kupelekwa Mahakama Kuu Rais Temer angesimamishwa kazi kwa muda wa siku 180 na spika wa bunge angekuwa rais wa kipindi cha mpito.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles