28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

BRELA yawanoa wadau wa biashara kuhusu wamiliki manufaa

Na Winfrida Mtoi, Mtazania Digital

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wadau juu ya kuelewa dhana ya wamiliki manufaa ‘Beneficial Owners’ kwa lengo  kuziwezesha kampuni kutuma taarifa sahihi.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Machi 14,2024 katika ukumbi wa hoteli ya Seashells, jijini Dar es Salaam yakihusisha mawakili, wafanyakazi wa benki, wafanyabiashara na wadau wengine wa biashara.

Akizungumza katika ufunguzi wa  mafunzo hayo, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Robert Makaramba ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema kampuni nyingi si rahisi kumfahamu mmiliki wa kampuni au ubia, hivyo kupitia warsha hiyo wadau watapata uelewa juu ya kuwasilisha taarifa zinazotakiwa.

Jaji Mstaafu Makaramba amesema dhana ya wamiliki manufaa  ni mpya na ilingia kwa kutumia sheria ya utakatishaji fedha, hatimaye imeingizwa kwenye sheria nyingine, ikiwemo sheria ya makampuni na uandikishaji majina ya biashara.

Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara BRELA, Isdor Nkindi,akitoa somo katika mafunzo ya wadau wa biashara kuhusu dhana ya wamiliki manufaa leo Machi 14,2024 jijini Dar es Salaam.

Amesema faida ya taarifa kuhusu wamiliki manufaa, inaimarisha biashara, kuvutia wawekezaji na kuondoa changamoto ya rushwa kwa sababu inahusu mmiliki halisi ambaye ni mtu.  

“Nawapongeza BRELA kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kuandaa warsha hii ambayo imekuja katika wakati  muafaka, ni matumaini yangu  washiriki wakitoka hapa watapata kile kitakachowaelewesha kuhusu wamiliki manufaa, amesema Jaji Mstaafu  Makaramba.

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Robert Makaramba(wa pili kushoto aliyekaa kwenye kiti) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa BRELA na washiriki wa mafunzo hao.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara BRELA, Isdor Nkindi amesema kutokana na  tathmini waliyofanya tangu kuanzishwa kwa sheria hiyo, bado kuna upungufu wa uelewa kwenye kuwasilisha taarifa ndiyo sababu wameamua kutoa elimu kwa wadau.

Ameeleza kuwa katika takwimu za sampo walizochukua 15,000 zilizowasilishwa, wamebaini upungufu wa uelewa wa dhana yenyewe na mipaka ya uwasilishaji ambapo zaidi ya asilimia 75 walikuwa wanafanya makosa katika ukokotoaji taarifa.

“Tunaendelea kuwajengea uwezo pale walipokwama na kuwaelekeza namna ya kuzirekebisha, tunatarajia kuanzia sasa na kwenda mbele, tunaamini taarifa zitakazofika kwa msajili zitakuwa zinasajiliwa moja kwa moja,” amesema Nkindi.

Amefafanua kuwa dhana ya wamiliki manufaa ilikuja  baada ya kuonekana kukuwa kwa kasi kwa makosa ya kifedha,iliyotokana na watu kujificha nyuma ya kampuni na makubalino, hivyo kushamiri makosa mbalimbali ikiwemo kupitisha fedha na bidhaa haramu.

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo,Grad Mutani, amesema wamejifunza jinsi ya kutambua kuwa mmiliki wa manufaa lazima awe na hisa kuanzia asilimia tano na kuwataka mawakili kusaidia kuweka uwazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles