25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

BONGO MUVI KABLA HAMJATOA LAWAMA REKEBISHENI HAYA

TUMEKUWA tukishuhudia tasnia ya filamu ikipita katika wakati mgumu kufuatia soko lake kuyumba. Soko la filamu limetikisika na kufanya wadau wakubwa wa sanaa kuanza kutafuta njia mbadala ya kurudisha hadhi ya kiwanda cha filamu.

Kumekuwa na visingizio vingi ambavyo kwa namna moja ama nyingine havina mashiko kutokana na ukweli kwamba matatizo yanaanzia kwa wasanii wenyewe hasa katika kazi zao.

Msingi wa biashara kwenye filamu unaanza ndani ya mwongozo wa filamu ambao msanii anaweka usanii wake kisha kitu kizuri kinapatikana na kufanya mashabiki wamiminike kununua filamu punde inapoingia sokoni.

Biashara haiwezi kuwa nzuri kama filamu haina hadithi iliyobeba burudani inayozingatia maadaili na elimu kwa watazamaji. Au hadithi inakuwa nzuri ila msanii anashindwa kuuvaa uhusika, hapo ndipo mastaa wengi walipopoteza mashabiki.

Kabla hatujatoa lawama ambazo tumezoea kuzielekeza kwenye serikali ni lazima turekebishe makosa ambayo kwa kiasi kikubwa yamepunguza mvuto wa mashabiki na kuzifanya filamu kutoka Korea kuwa nambari moja sokoni.

Je mnataka serikali iwaandalie myongozo bora ya filamu? Mnataka Waziri aingie ‘location’ kuwaongoza wasanii ili filamu zetu ziwe bora kuliko zile zinazo tafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na kuuzwa kwa bei rahisi kule kitaa? Hapana.

Ni lazima turekebishe hizi kasoro ndogo ndogo zilizopelekea soko la filamu kuporomoka ili serikali ikiweka nguvu katika yale mambo makubwa ya kisera tasnia hii iweze kusonga mbele kwa kasi kubwa.

Serikali tunahitaji iweke nguvu kwenye mambo makubwa  kama kuwawezesha wasanii kupata mitaji mikubwa itakayofanya wafanye kazi zenye ubora. Kutengeneza mazingira rafiki ya kusambaza kazi za wasanii wetu.

Hali kadharika kuweka sheria kali za kudhibiti wizi wa kazi hizo. Hayo ni majukumu ya serikali lakini hayawezi kutekelezeka kama wasanii wenyewe hawajawa tayari, hawajarekebisha mapungufu kwenye kazi zao yaliyoleta.

Kabla pumzi haijakata ni lazima wasanii na wadau wakubwa wa filamu wajitazame wao kwanza ndiyo waanze kutoa lawama lakini kwa mwendo huu wa kutoa lawama bila kujitathimini tutakuwa tunapoteza wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles