28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

JANUARI IMESEPA HATUTAKI KISINGIZIO KINGINE

NA RAMADHANI MASENGA

WABONGO tumejaliwa sifa ya kulaumu. Nenda katika nyanja zote, mbongo hata akiwa anajua kitu fulani huwa hashauri ila yeye analaumu tu.

 Moja kati ya miezi ambayo huwa tunailamu bila sababu za msingi sana ni mwezi uliopita wa Januari. Wengi tunauita mwezi dume. Katika mwezi huo kila mmoja analalamika hana hela maisha magumu.

  Kila mmoja atakwambia Desemba imemwacha mweupe kutokana na sikukuu mfululizo na mwezi wa kwanza ukaingia na mambo ya ada za shule na wengine wasio na nyumba watakwambia wenye nyumba wamekomba zote na kuwaacha weupe.

Ila swali la msingi hapa ni kwanini kila Januari tunalalamika tu, kwani huu mwezi huwa unakuja kwa kutuvizia?

Kama hoja ni kuwa  sikukuu zilizopangana za Desemba zinatufanya tumalize mpunga wetu wote, sasa kwanini tusibadili aina ya kuzisherehekea? Kwani ni lazima kila sikukuu kuipa uzito sawa na sikukuu zingine? Hiyo mosi.  

Ila pili ni kwanini wakati tukikaribia Desemba tusiwe makini katika suala la matumizi ya fedha ili tuweze kujikusanya vema miezi mingine ili  Desemba na Januari zitukute na unafuu mkubwa? Wabongo hatupendi mikakati, sisi kazi yetu kulaumu tu.    

Kwa kuendendekeza uboya huu  wa kulaumu, sasa kila mtu analalamika maisha magumu. Eti hata yule ambaye hakuwa na mchongo wowote, deile tulimuona kitaa akipiga mizinga na kuanua nguo asizozianika yeye na yeye analalamika laifu taiti. Sasa unategemea laifu liwe softi kwako wakati hutaki kazi yoyote zaidi ya kushinda maskani kujadili politiksi tu? Kwa kulaumu wabongo tumejaaliwa.

Honestly suala la Januari huwa linanichefua kichizi. Ukiona namna watu wanavyolalamika juu ya mwezi huu utadhani mwezi huu huja mara moja kati ya miaka kumi ama huja kwa kutuvizia.

Huu mwezi ni wa kila mwaka, sasa kwanini miezi mitatu ama minne kabla ya Desemba tusiwe na matumizi ya adabu na maadili ili ikifika Desemba kisha Januari tuwe tunatiririka tu? Hili wabongo hatutaki, tunasubiri Januari ifike tuangalie tumlaumu nani, hahaha noma sana.

Ila uzuri wa Januari kuna heshima kubwa imepatikana. Hata wale mademu wanaokataaga ukiwahonga buku mbili, walikuwa na heshima.

Kuna mmoja alimuomba jamaa yangu elfu kumi ila jamaa akasema hawezi kutoa mahela mengi, hivyo ila anaweza kutoa buku mbili, demu yule mwenye nyodo, ambaye miezi kadhaa iliyopita alikuwa akisema anataka mwanamume mwenye uwezo wa kumhonga kuanzia laki moja na zaidi, alipokea buku mbili kwa heshima utadhani ndiyo ilikuwa imeshikilia roho yake.

 Heshima ilipatikana aisee. Maeneo ya Bar na Pub zote wale wenye kupenda bia za kibishoo walibadili gia angani na kuendelea kula vitu vigumu.

Ila cha kuchekesha zaidi ni kuwa wabongo huwa hatufundishwi na matukio hata kidogo. Baada ya Januari kupita watu hawajapata funzo la umuhimu wa kusevu mavumba wala kuwa na matumizi sahihi ya mkwanja.

 Kwa kuonesha hivyo, eti baadhi walikesha tarehe 31 kuamkia mwezi wa pili wakikata vyombo kwa kile walichodai na furaha ya kuachana na mwezi uliojaa mateso na nuksi, hahaha wabongo noma sana aisee.

 Ebwana eeeh kama vipi mida wana, naenda kujipanga vema ili nisiwe kama ninyi deile kulalamika tu hahahaha, sitakagi ujinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles