29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Blxckie ang’ara Africa Rising

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MSANII chipukizi mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni rapa na mtayarishaji wa muziki kutoka Durban, nchini Afrika Kusini, Sihle Sithole ‘Blxckie’ ametangazwa na Kampuni ya Apple Music kama msanii wa hivi karibuni wa Africa Rising.

Akizungumza baada ya kupewa shavu hilo, Blxckie anasema: “Kwa hakika hii ni kubwa kwangu! Nimeheshimiwa kutambuliwa kama msanii mpya wa Africa Rising.

“Nyuso za tasnia ya muziki ulimwenguni zinabadilika haraka kutokana na majukwaa na huduma kama hii kwenye Apple Music. Kwangu na muziki wangu kuchaguliwa ni kama jukumu muhimu katika historia yangu. Nataka wale ambao wameiamini B4now, sasa wajivunie. Acha tuifanye Afrika iinuke!”

Baada ya kutawazwa mshindi wa mashindano ya Studio Sessions mwishoni mwa mwaka 2020, Blxckie aligunduliwa kama nyota wa baadaye, baada ya kujenga jamii yake ya Hip Hop, pamoja na waimbaji wenzake na washirika Lucas Raps, Dr Peppa, FLVME, LeoDa Leo, Yuang na 808 Sallie.

Blxckie anawakilisha wimbi jipya la wanamuziki ambao wote ni zao la mizizi yao na pia tamaduni kuu na nguvu na msisimko wake umeleta nguvu mpya katika Muziki wa Hip Hop nchini Afrika Kusini.

Ngoma mpya kali za Blxckie zinapatikana hapa kwenye Apple Music:  https://open.spotify.com/playlist/2vZ7pVRuwZDvSmqo6NEgSJ

Africa Rising ni miongoni mwa mipango mipya mingi ya Apple Music kutafuta, kusaidia na kuinua vipaji vya wasanii wa Afrika na kuwatangaza ulimwenguni.

Mpaka sasa inapatikana katika nchi 33 Afrika, inatangazwa zaidi na Africa Now Radio chini ya mtangazaji LootLove ambaye amefanya makala na wasanii kama Tiwa Savage, Yemi Alade, Cassper Nyovest, Mr Eazi, Patoranking, Rayvanny, Kiddominant, Mayorkun, Fireboy DML, Adekunle Gold, Master KG na Yaw Tog.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles