27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Bitchuka, Sikinde kutumbuiza Siku ya Msanii kesho

Bitchuka,NA MWANDISHI WETU

MWANAMUZIKI mahiri nchini, Hassan Rehani Bitchuka, leo ataongoza kikosi kamili cha bendi ya Mlimani Park Orchestra kutoa burudani katika onyesho la kazi za wasanii katika viwanja vya Makumbusho, Posta, jijini Dar es Salaam.

Maonyesho hayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea Tuzo za Siku ya Msanii, iliyozinduliwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene.

Mlimani inakuwa bendi ya pili kubwa kupanda kwenye jukwaa la Msanii mwaka huu, ikitanguliwa na African Stars ‘TwangaPepeta’ ambayo ilitumbuiza jana sambamba na kikundi cha Ifakara Band, Safi Theater.

Meneja wa Uhusiano wa Siku ya Msanii, Petter Mwendapole, alisema Mlimani wamealikwa kushiriki tamasha hilo kwa kutambua mchango wao katika fani ya muziki na mambo mbalimbali ya jamii.

“Tumeita wasanii chipukizi na wakongwe ili waweze kufanya kazi pamoja katika jukwaa la Siku ya Msanii, hii itawasaidia wasanii chipukizi kujifunza, lakini pia wakongwe kutia darasa kwa chipukizi katika kunyanyua muziki,” alisema.

Akizindua maadhimisho hayo, Mwambene aliwataka wasanii watambue thamani yao na kutumia fursa wanazozipata katika kujiendeleza.

Siku ya Msanii inaandaliwa na kampuni ya Haak Neel Production (T) Ltd kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles