TAMASHA la ‘The Beat’ lenye lengo la kukutanisha wasanii na wadau mbalimbali wa muziki ndani na nje ya nchi linatarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa Paparazzi Bistro Club – Slipway, jijini Dar es Salaam.
Katika tamasha hilo jipya baadhi ya wasanii watakaolinogesha ni pamoja na mkali wa Bongo Fleva, Mzungu Kichaa, mkali wa nyimbo za asili, Samweli Hokororo, Ifa Band na mwanamuziki Banana Zorro, ambao watatumia bendi kupiga muziki wa moja kwa moja.
Wasanii wote wamejipanga kuja kufanya muziki mzuri kwa mafanikio makubwa ya kukuza muziki huo ambapo Ifa Band, Samuel Hokororo, aliyeanza kuimba akiwa na miaka nane wakati alipokuwa shule, nyumbani na alipokuwa kanisani na kufanikiwa kutumbuiza katika Tamasha la Sauti za Busara ameahidi makubwa katika tamasha hilo.
Pia Banana Zorro baada ya kuimba nyimbo nyingi za bongo fleva kwa mafanikio, baadaye alianzisha B Band, naye amesisitiza kwamba amejipanga kutoa burudani ya kutosha kupitia muziki na sauti yake ambayo ndiyo kivutio kwa mashabiki wake pamoja na Mzungu Kichaa anapiga gitaa na kuimba kwa Kiswahili na Kiingereza ambaye ndiye mwandaaji wa tamasha hilo, wameahidi kutumbuiza nyimbo zao mpya na kutoa somo la muziki kwa watu wote watakaohudhuria tamasha hilo.
Tamasha hilo limedhaminiwa na Caravan Records na Goethe Institute Tanzania.