27.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

BILL GATES KUWA TRILIONEA WA DUNIA

WENGI wanadhani utajiri wa Bill Gates umefika kikomo na kwamba atakuwa bilionea pekee. Hivi unadhani Bill Gates utajiri wake unaishia kwenye ubilionea? Je, ni kwa vipi Bill Gates atazidi kupata utajiri hadi kuwa Trilionea?

Katika nyakati za maisha yetu upo uwezekano wa kushuhudia Trilionea wa kwanza duniani, ambaye ni Bill Gates mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft.

Kwa mujibu wa uchambuzi mpya wa masuala ya kibiashara uliotolewa na Televisheni ya CNBC kupitia kipindi chake cha ‘Masoko Leo’, ambacho kimetumia takwimu za Shirika la Kimataifa la Oxfam na kubainisha Gates anatarajiwa kuwa raia wa kwanza wa Marekani kuwa Trilionea.

Gates mwenye umri wa miaka 61, alitajwa na jarida la Forbes kumiliki utajiri wenye thamani ya dola bilioni 84 hivyo kuwa kinara wa mabilionea wengine duniani. 

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Oxfam linalojihusisha na mapambano ya kukabiliana na umasikini duniani, limesema tangu mwaka 2009 wastani wa utajiri wa Bill umekuwa ukiongezeka kwa asilimia 11 kila mwaka 2009.

Mathalan, utafiti wa Oxfam uliotolewa  hivi karibuni na kubainisha kuwa mabilionea 8 duniani wanamiliki utajiri mkubwa kuliko idadi ya watu bilioni 3.6 ambao nusu yao ni masikini.

Ripoti hiyo ilibainisha kuwa kati ya mabilionea hao wapo ambao utajiri wao unazidi kuongezeka zaidi, hali ambayo inatarajiwa kumshuhudia trilionea wa kwanza katika kipindi cha miaka 25 ijayo wakati ambapo Bill Gates atakuwa na umri wa miaka 86.

Kwa mujibu wa Oxfam, wakati Gates alipoachia ngazi Microsoft mwaka 2006, utajiri wake ulikuwa dola bilioni 50. Hadi mwishoni mwa mwaka 2016 utajiri wake uliongezeka hadi dola bilioni 75.

“Licha ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kupitia taasisi yake ya Melinda and Gates kusaidia watu mbalimbali duniani,”  ilisema ripoti ya Oxfam.

Aidha, shughuli za kusaidia watu wasiojiweza zinazofanywa na Gates kupitia taasisi yake binafsi, pia ni miongoni mwa waanzilishi wa asasi ya The Giving Pledge ambayo inahusisha baadhi ya matajiri kutoa misaada binafsi ambayo inatokana na nusu utajiri wao.

Kwa uchambuzi wa kisayansi, utafiti wa Oxfam, unaweza kutumika kupata wastani wa ukuaji au ongezeko la utajiri na matarajio yanayoonyesha faida, kutoka asilimia 11 ya mwaka 2009 hadi kiwango cha sasa cha utajiri wa Gates (ambacho ni zaidi ya dola bilioni 84 kwa mujibu wa Forbes).

Endapo uwekezaji huo utaendelea kuimarika kama ilivyo awali pamoja na matarajio, Gates mwenye umri wa miaka 61 atakuwa trilionea wa kwanza Marekani na duniani.

“Kulingana na mazingira hayo, ukishakuwa tajiri, unatakiwa kujaribu kupambana kupata utajiri zaidi ya ulionao,” ilisema ripoti ya Oxfam.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles