26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Bilioni 28 kulipa fidia watakaopisha bomba la mafuta kutoka Uganda

Na Yohana Paul, Geita

TAKRIBANI Sh bilioni 28 zinatarajiwa kutumika kutoa malipo ya fidia kwa wananchi 10,516 nchi nzima watakaopisha utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi  (EACOP) kutoka nchini Uganda hadi mkoani Tanga.

Maafisa wa Serikali Mkoani Geita wakipatiwa semina juu ya mradi wa bomba la mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.

Hayo yameelezwa jana na Mratibu wa Mradi huo nchini, Asiadi Mrutu wakati wa semina kwa maafisa wa Serikali mkoani Geita iliyolenga kulenga kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi, kujadili ushirikishwaji wa wananchi sambamba na kujadili fursa za mradi huo.

Mrutu amesema fidia ya mradi huo ipo katika makundi mawili, kwanza ni maeneo ya yatakapojengwa makambi 14 na takribani wananchi 394 watalipwa fidia ya Sh bilioni 2.5 na kundi la pili ni watakaopisha mkuza wa bomba na wananchi takaribani 9,122 watalipwa fidia ya Sh bilioni 25.


Alieleza kuwa hadi kufikia Julai 30, mwaka huu fidia imekwishalipwa kwa wilaya za Nzega, Igunga, Singida ambapo jumla ya watu 44 wamelipwa kiasi cha Sh 381,703,273 na taratibu za uhakiki, utoaji elimu, mikataba na kibenki zinaendelea kulipa fidia kwa waliobaki.

Mrutu amesema serikali imekwisha toa Sh bilioni 259.96 ikiwa ni mchango wake kama mwanahisa wa EACOP kwani asilimia 80 ya mradi sawa na kilomita 1,147 kati ya kilomita 1,443 za urefu wa bomba zipo upande wa Tanzania na litapita kwenye mikoa nane.

Aliongeza, bomba hilo linatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafirisha lita 216,000 za mafuta ghafi kwa siku na kujaza matenki 216 ambapo ujenzi wa mradi unatarajiwa kutumia dola za kimarekani bilioni 3.5 sawa na Sh tillioni kwa fedha za kitanzania.

“Mikoa ambayo itapitiwa na mradi huu ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga na itasaidia ongezeko la sekta ya uwekezaji kwa zaidi ya asilimia 60 sambamba na kutoa ajira mbalimbali kwa Watanzania.

“Kiwango cha chini cha makadirio ya ajira kwa watanzania ni nafasi za uongozi kwa kampuni ya EACOP itakayozalisha ajira kwa asilimia 15, kazi za kitalaamu itazalisha ajira kwa asilimia 30 na kazi zisizo za ujuzi na utaalamu itazalisha ajira kwa asilimia 70, kipaumbele kikiwa ni kwa wazawa,”amesema.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Herman Matemu alitoa wito kwa wananchi wote kutumia fursa za kiuchumi zitakazotokana na mradi huo na kuachana na tabia za wizi na udokozi wa vifaa kwani serikali inapojenga miradi tofauti inalenga kukuza uchumia wa taifa hivyo itawachukulia hatua wote watakaoihujumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles