29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Bilionea China jela miaka 18

Beijing, China

MFANYABIASHARA maarufu China, Sun Dawu, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani, ikiwa ni mwendelezo wa Serikali ya nchi hiyo kuwashughulikia wakosoaji wake.

Sun mwenye umri wa miaka 67, ambaye ni bilionea aliyewekeza zaidi kwenye bidhaa za kilimo katika Jimbo la Hebei, amekuwa akipaza sauti kulaani ukandamizwaji wa haki za binadamu nchini humo.

Katika mashitaka yaliyokuwa yakimkabili, mfanyabiashara huyo alitajwa kuhatarisha hali ya utulivu, kupora mashamba, kuratibu vikundi vya kushambulia watumishi wa umma, sambamba na kuizua Serikali kufanya kazi zake.

Mbali ya kifungo, pia Sun ameshurutishwa na mahakama kulipa faini ya Dola za Marekani 478,697

Mwaka jana, ilielezwa kwamba yeye, ndugu zake 20, na washirika wake wa kibiashara wanashikiliwa na vyombo vya dola kwa kile kilichoripotiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi. Kipindi hicho, aliibuka na kuliambia Shirika la Habari la AFP wafanyakazi wake wamejeruhiwa na polisi.

Hii si mara ya kwanza kwake kuhukumiwa kifungo cha gerezani kwani ilikuwa hivyo mwaka 2003 lakini aliachiwa baada ya wanaharakati na raia kupaza sauti za kumkingia kifua.

Hukumu ya safari hii ni mwendelezo wa China kuwakalia kooni wafanyabiashara wakubwa, hasa wanaikosoa Serikali, ikikumbukwa kuwa tayari kampuni za Alibaba, Didi na Tencent zinachunguzwa zikihusishwa na makosa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles