20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

BIFU LA MOBETTO, ZAMARADI NI MSHONO AU KUNA KINGINE?

Na SWAGGAZ RIPOTA


UNAWEZA kujiuliza chanzo cha vita ya maneno iliyozua gumzo wiki hii kwenye tasnia ya burudani Bongo kati ya mastaa Zamaradi Mketema  na Hamisa Mobetto imesababishwa na mshono wa gauni na si jambo jingine?

Moto wa bifu hilo ulianza kuwaka pale mtangazaji Zamaradi alipozikanusha tuhuma za kudhulumu fedha zilizodaiwa kuchangishwa kwa watu ili kufanikisha sherehe ya 40 ya mwanaye Salah, wiki mbili zilizopita.

Zamaradi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa kituo cha runinga cha Wasafi TV kinachomilikiwa na Diamond Platnumz, anasema 40 ya mtoto wake ilikuwa na wadhamini kibao ambao walifanikisha na hakukuwa na mtu hata mmoja aliyechangishwa fedhaa kama ambavyo imezushwa.

Bifu hilo jipya mjini liliendelea kupamba moto baada ya Hamisa Mobetto kuingiza ishu ya gauni ambapo alimjibu Zamaradi kwa kuweka wazi mazungumzo yao ya siri waliyoyafanya kupitia Instagram (DM) juu ya makubaliano yao kuhusu Mobetto kumshonea gauni alilolivaa kwenye sherehe ya 40 ya mwanawe Salah.

Licha ya kufanya makubaliano hayo mpaka Mobetto kununua vitambaa kwa ajili ya kushona gauni ambalo  Zamaradi alimwagiza amshonee ikiwamo kumpa aina ya mshono anaoutaka, mtangazaji huyo alikwenda kushona gauni kwa fundi mwingine kutokana na kupishana kwa muda.

Zamaradi amemjibu shabiki mmoja aliyemuhoji sababu za kumpa mshoho mwanamitindo Hamisa Mobetto kisha kwenda kushona kwa fundi mwingine akisema: “Mwanzo nilitaka kushona kwake (Mobetto) ila tukapishana siku ambayo alikuwa anapatikana mimi sikupatikana siku niliyokuwa napatikana yeye hakuwepo, nikalazimika kwenda kwa fundi mwingine karibu na kwangu nyumbani Salasala ambaye niliona anaweza kunitolea kitu kama hicho.”

KWA HABARI ZAIDI PATA NAKALA YAKO LA GAZETI LA MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles