29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Bifu la Lil Wayne, Birdman linavyogonganisha mastaa

Lil Wayne
Lil Wayne

Na FARAJA MASINDE,

RAPA Lil Wayne ambaye imekuwa stori ya zaidi ya mwaka mmoja sasa kwenye ulimwengu wa Hip Hop hasa baada ya kuwa na bifu zito na rapa Birdman ambaye ndiye mwanzilishi Lebo ya Cash Money Records.

Bado stori kwenye bifu hilo zinaendelea kwani kila kukicha mapya yanazidi kuibuka kati ya pande hizo mbili zinazovutana huku kigezo kikubwa kikiwa ni masilahi baina yao.

Chanzo cha ugomvi huo ni baada ya Wayne kutaka kulipwa kiasi cha Dola milioni 51 na Birdman na Cash Money anazowadai.

Kwa sasa kuna taarifa mpya kuhusiana na bifu hilo ambapo inaelezwa kuwa, Wayne huenda akapewa mkwanja wake wote anaomdai Birdman.

Huu ni ujumbe uliotolewa na James Prince ambaye ameamua kuingilia kati kwenye bifu hilo lililodumu kwa muda mrefu baina ya Wayne na Birdman ambaye ni baba wa kufikia.

Prince, ambaye ni bosi wa Rap-A-Lot Records na anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa, amesema kuwa anafikiri huu ni wakati mwafaka wa yeye kujihusisha kwenye bifu hilo linalotishia kuupoteza muziki wa Wayne.

Prince anasema inasikitisha kuona kuwa, Wayne amefikia hatua ya kutangaza kuacha muziki kutokana na vita ya masilahi baina yake na Cash Money.

Hatua hiyo imeonekana kumkera Prince na kuhisi huenda Lil Wayne amekuwa akionewa kutokana na upole wake, hivyo yuko tayari kutumia uimara wake binafsi kwa ajili ya kutafuta masilahi ya Wayne.

“Naamini kabisa kuwa tukishirikiana tunaweza kurejesha fedha za Wayne anazowadai Cash Money.

“Natambua kuwa kuna wengi ambao wanaangalia ugomvi huu kwa karibu lakini hawataki kujionyesha hivyo binafsi nimeona sina cha kusubiri, siwezi kusubiri mpaka mambo yaharibike ndipo nitokee kwani dhumuni ni kupata ufumbuzi,” anasema Prince ambaye mtoto aitwaye  Jas Prince ndiye aliyemuibua Drake na kumuweka pamoja na Lil Wayne na Young Money.

Kwa namna hiyo huenda Wayne akapata mkwanja wake na labda akabadili uamuzi wake wa kuacha muziki kwani familia ya Prince inapoamua kuingilia kati jambo huwa halishindikani, hivyo ni wazi kuwa huenda ikafanikiwa kuwaweka pamoja Wayne na Birdman.

Inaelezwa kuwa, kwa vipindi tofauti, Wayne amekuwa akisikika akisemakuwa familia ya Rap-A-Lot iliyochini ya Prince kuwa ipo nyuma yake.

Masta Kopi ‘Carter V’

Kwenye upande mwingine wa shilingi, Birdman ameweka wazi kuwa Master Kopi ya album mpya ya Wayne, ‘Tha Carter V’ anayo mwenyewe na hajawapa Cash Money ndiyo maana hawawezi kuitoa.

Kauli hii ya Birdman imetoka ikitafsiriwa kama majibu kwa Wayne ambaye amesema kwamba hatakaa afanye kazi na Birdman.

“Nastaafu kwa ajili ya Birdman lakini vitu vinaweza kubadilika.

Wayne alitoa majibu hayo baada ya kuandamwa na maswali kutoka kwa mashabiki wake waliokuwa wakijua kuwa ni kweli atastaafu muziki au la kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

Wayne amekuwa akilalamika kuwa, Birdman ana mamilioni ya fedha anayomdai ambapo kukosa fedha hizo kumesababisha madhara kwenye maisha yake binafsi.

“Nina familia kwa maana ya watoto, nina mama yangu pia, nahitaji kulipia bili na hii ndiyo biashara yangu,” anasema Wayne.

Wayne anasema kuwa kamwe hataweza kuja kufanya kazi na Birdman tena maishani mwake  na hivyo kwa makusudi na dhamira ya dhati anaona ni bora astaafu muziki labda mpaka pale atakapolipwa fedha zake.

Rapa huyo amekuwa akituma meseji kwa aliyekuwa bosi wake wa zamani na kumwambia kuwa yeye ni mgodi hivyo ana kila sababu ya kutembea akiwa huru.

Wayne amesema kuwa hayuko tayari kurejea tena kwenye muziki kwani anadhani hafikirii kama anaweza kurudi na kufikia mafanikio aliyowahi kuyafikia kwenye muziki huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles