21.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

BEYONCE AKANUSHA KUWA MJAMZITO

NEW YORK, MAREKANI

WIKI kadhaa zilizopita staa wa muziki wa Pop nchini Marekani, Beyonce, aliripotiwa kuwa na ujauzito kutokana na muonekano wa tumbo lake, lakini mrembo huyo amekanusha kupitia video inayosambaa akiwa analionesha tumbo hilo.

Msanii huyo kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki na mume wake Jay Z, ambayo inajulikana kwa jina la ‘On The Run II Tour’ hivyo katika ziara hiyo amekuwa akiwashangaza mashabiki kutokana na nguo anazovaa na kuwafanya mashabiki wadhani kuwa anatarajia mtoto wa nne.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aliposti video yake akionesha tumbo na kusema, “Nadhani hapa ninaonekana vizuri kwa kila mmoja, taarifa zilisambaa kudai kuwa nina ujauzito, lakini ni wazi kwamba hakuna ukweli wa namna hiyo,” aliandika.

Beyonce na Jay Z, kwa sasa wana jumla ya watoto watatu, wakwanza akijulikana kwa jina la Blue Ivy Carter mwenye umri wa miaka sita, pamoja mapacha Rumi Carter na Sir Carter wenye umri wa mwaka mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,813FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles