20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

WIZKID KUMLETA P.DIDDY NIGERIA

LOS ANGELES, MAREKANI

STAA wa muziki nchini Nigeria, amezidi kujipenyeza katika muziki wake kuhakikisha unafika mbali baada ya mwishoni mwa wiki iliopita kuonekana akiwa nyumbani kwa rapa P.Diddy na kufanya naye mazungumzo.

Baada ya wawili hao kukamilisha kufanya mazungumzo, P.Diddy aliposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiweka wazi kuwa amezungumza na msanii huyo na kumuhakikishia kuwa atakuja nchini Nigeria.

“Wizkid alinitembelea nyumbani kwa ajili ya kuja kuniona, kuna mambo ameniambia yamenifurahisha sana na nimeyapenda kutoka nchini Nigeria, hivyo nataka mashabiki wajue kwamba nitakuja nyumbani Nigeria, haitochukua muda mrefu nitakuja,” alisema P.Diddy.

Wizkid yupo nchini Marekani kwa ajili ya ziara yake ya muziki, hivyo ameonekana akiwa na mastaa mbalimbali kama vile rapa Drake, DJ Khaled, prodyuza Metro Boomin pamoja na Fergie, hivyo ziara hiyo inaweza kuwa na mafanikio makubwa kwa staa huyo wa Nigeria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles