25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Benki UBA yaja na ushauri kwa taasisi za fedha

Na  MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

TAASISI  za fedha nchini, zimeshauriwa kubadilika katika kuwahudumia wateaja wao na kuacha kutoa huduma kwa mazoea  wakati wanapotoa huduma kwa  wateja wao, ili kuendana na kasi pamoja na ushindani uliopo kipindi hiki cha mabadiliko ya teknolojia ili kuweza kufanya vizuri kwenye soko la ushindani.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA-Tanzania,  wakati  benki hiyo ilipoungana pamoja na wateja wake katika kusherehekea wiki ya wateja duniani iliyofanyika tawi la Nyerere.

“Nashauri taasisi zinazotoa huduma za kifedha lazima zibadilike na kuacha kutoa huduma kwa mazoea badala yake ziwe na ubunifu unaoendana na kipindi hiki cha ushindani wa soko la teknolojia kwani usipofanya hivyo ushindani ni mkubwa sana,” alisema Isiaka

Alisema UBA wanayo furaha kuungana na wateja wao kusherekea siku ya huduma kwa mteja duniani kwa kuwa wao ndio wanafanya benki hiyo kuwepo na kuendelea kutoa huduma stahiki na zenye ubora kwa wateja wao kwenye matawi yao yote nchini .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ledgewood Investiment, Raymond Mubayiwa, alisema kuwa katika kipindi hiki cha kusherekea wiki ya huduma kwa wateja wamejifunza mengi ikiwamo kupata fursa ya kukutana na watoa huduma wao na kuzungumza nao kwa kina kuhusu masuala mbalimbali jambo ambalo kwao limewapa faraja kubwa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles