KIZIMBANI KWA UBAKAJI MTOTO WA MIAKA 9

0
741

ERICK MUGISHA – DAR ES SALAAM

MKAZI wa Ilala Mchikichini, Ramadhani Kwivamba (43), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akidaiwa kubaka Binti wa Miaka 9. 

Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri, Ellen Masulali, akimsomea mashtaka mtuhumiwa mbele ya Hakimu Ester Mwakalinga, alidai Julai 26 mwaka huu, akiwa Kijitonyama Wilayani Kinondoni, Dar es salaam alimbaka Binti wa miaka 9.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri Masulali alidai Upelelezi hauja kamilika na kuomba tarehe nyingine kwa kutajwa kwa kesi hiyo.

Hakimu Mwakalinga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho vya Taifa.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti na kesi take itatajwa tena octoba 22.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here