27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Belle 9: Umaarufu wa Masogange umetokana na mimi

Belle 99NA THERESIA GASPER

MSANII wa RnB kutoka mji kasoro bahari, Morogoro, Abednego Damian ‘Belle 9’, ameweka wazi kwamba umaarufu wa mkali wa kunogesha video za wasanii nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’, umetokana na wimbo wake wa ‘Masogange’.

Akizungumza juzi alipotembelea Ofisi za New Habari Limited (2006) zinazochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba na Rai, Belle 9 alisema huwa anaamini kipaji cha mtu ndio maana wengi aliowashirikisha katika nyimbo zake wamepata umaarufu mkubwa.

“Nimefanya kazi na wasanii wasiotambulika akiwemo Masogange na wamepata umaarufu mkubwa pia nimefanya kazi na maprodyuza wengi wasiojulikana lakini baada ya kazi hizo wamejulikana, hivyo huwa sidharau uwezo wa mtu ninachoangalia ni ubora wa kazi zake na si jina lake hata kama ni chipukizi,” alisema.

Kati ya video alizofanya na waongozaji wasio na majina makubwa na zimefanya vizuri ni ‘Burger’ na ‘Movie Self’ inayotarajiwa kuachiwa kesho ambayo ameshirikiana na wasanii Izzo Bizness, Jux, Mr Blue, G. Nako na Nandy.

“Audio ilishatoka ilifanywa na mtayarishaji Tuddy Thomas huku video ikiwa chini ya prodyuza chipukizi QG kutoka Morogoro, naamini kazi yake mtaifurahia,” alimaliza Belle 9.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles