30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Beki Simba ajipa likizo timu ya Taifa

abdi-banda-390x390NA ZAINAB IDDY

BEKI wa Simba, Abdi Banda, amesema kuwa kwa hivi sasa hana mpango wa kuitumikia timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ hadi baada ya mwaka mmoja kutokana na majanga aliyokutana nayo akiwa na timu hiyo.

Banda hivi karibuni ameanza mazoezi na kikosi chake cha Simba, baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la nyama za paja alilolipata akiwa na Taifa Stars kipindi ikijiandaa na michuano ya Afcon ilipokuwa kambini nchini Uturuki.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Banda alisema kutokana na matatizo hayo hana mpango wa kuitumikia tena kwa miaka ya hivi karibuni.

Alisema moja ya vitu vilivyosababisha kumrudisha nyuma kisoka ni majeraha ya mara kwa mara aliyokuwa akiyapata akiwa Stars.

“Watu wanaweza kusema sina uzalendo na nchi yangu lakini nimejiwekea malengo ya kutoitumikia timu yoyote ya taifa kwa miaka ya hivi karibuni kwani ni moja ya vitu vilivyonirejesha nyuma.

“Hivi sasa napigania kurejea katika ubora wangu kama nilivyokuwa Coastal Union na Simba katika kipindi cha mwanzo, kisha kuanza mipango ya kwenda kucheza soka la kulipwa ambayo ilisimama kutokana na majeraha ya mara kwa mara niliyokuwa nikiyapata,” alisema Banda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,391FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles