25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Bashiru: Ushindi huu ni mzigo mzito kweetu

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

KATIBU Mkuu wa CCM, Dk.Bashiru Ally amesema wanachama  wa chama hicho wapokee ushindi wa Rais Dk.John Magufuli kama mzigo mkubwa kwao.

Amesema ushindi huo, ni mzigo kutokana na kupata ushindi wa kishindo ambao wanapaswa kutekeleza kila ahadi waliotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Alitoa kauli hiyo jijini Dodoma jana, baada ya Dk. Magufuli kukumkabidhi   cheti cha ushindi na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Semistocles Kaijage

Alisema wana jukumu la kuzisimamia Serikali zote mbili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.

“Niwaombe wana CCM, waupokee ushindi huu kama mzigo kama dhamana kubwa kama deni alivyosema Rais… katika ilani yetu tuna sura ya 10 ambayo inayotutaka kuanza kuzisimamia Serikali ambazo zimepewa  dhamana kwa sababu mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa uchaguzi ujao.Wakati tunapongezana  tujue kwamba tunaowajibu wa kuisimamia Serikali zote mbili ili tutimize ahadi zote,”alisema.

Alisema ushindi waliupata umebeba dhamana ya uchapa kazi pamoja na amani ambayo imeendelea kuwepo nchini.

“Ushindi tuliupata ni ushindi unaotubebesha dhamana ya kuchapa kazi ni ushindi kwa amani yetu kwa umoja wetu pamoja na mahusiano yetu,”alisema.

Aliwataka Watanzania wasikubali kuchonganishwa,kugombanishwa, badala yake kipindi hiki wanatakiwa kushikamana ili kulinda amani ya nchi.

“Nawaomba tushikamane kipindi hiki, kazi tuliyoifanya ni kubwa mafanikio tuliyoyapata ni makubwa, mshikamano wetu ndiyo nguzo yetu tusikubali kwa namana yoyote, tusikubali kuchonganishwa,tusiukubali kugombana na kuchukiana kwa sababu kufanya hivyo tutakuwa hatuwaenzi waanzilishi wa  taifa hili,”alisema.

Alisema siri ya  chama chake kuibuka na ushindi mkubwa katika nafasi za urais,ubunge na udiwani, imetokana na umoja.

“Na siri kubwa iliyotupa ushindi ni umoja wetu kwa mara ya kwanza tumeingia katika uchaguzi tukiwa wamoja na tumemaliza tukiwa wamoja na tumeheshimiana niwaombe wasianze kushehereka kwamba kazi imeisha sasa kazi ndio imeanza.

 “Tunahitaji kuwajibika, niwaombe madiwani wabunge wazingatie nidhamu ya chama tayari tunayomifumo tusianze kulindana kwa sababu ina gharama kubwa kwani  deni hili itabidi tujieleze mwaka  2025,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,454FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles