27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Augustino Vocal aanza kuachia ‘Kesho Yangu’

MINNESOTA, MAREKANI

BAADA ya kimya cha muda mrefu, mwimbaji wa Kimataifa anayeishi Marekani, Augustino Vocal, amerudi kivingine kwa kuachia wimbo, Kesho Yangu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Augustino alisema wimbo wake, Kesho Yangu ni moja kati ya nyimbo tatu alizopanga kuzitoa baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu hivyo mashabiki wajiandae kuzipokea na kumpa sapoti kama kawaida.

“Kwa kukaa kimya muda mrefu nikaona bora nije upya kwa nyimbo tatu za Injili, nimeanza na hii Kesho Yangu ambayo muda wowote kutoka sasa itakuwa kwenye chaneli yangu ya YouTube na nyingine zinakuja kwahiyo kama kawaida yako wewe shabiki, ndugu na rafiki yangu endelea kuwa karibu na kurasa zangu za mitandao ya kijamii,” alisema Augustino.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles