24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

BARAZA LA WADHAMINI CCM LAKABIDHIWA USIMAMIZI MAPENDEKEZO MALI ZA CHAMA

Na AGATHA CHARLES


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amelipa Baraza la Wadhamini la chama hicho jukumu la kusimamia mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi wa mali za chama hicho.

Dk. Bashiru alifanya hivyo jana, wakati Baraza hilo la kwanza linaloongozwa na Mwenyekiti wake, Anna Abdallah, kufika Ikulu Dar es Salaam, ambako walifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli.

Dk. Bashiru ambaye alikuwa Mwenyekiti wa tume iliyoundwa kuhakiki mali za chama hicho, iliyowasilisha ripoti yake Mei 21, kwa Dk. Magufuli, alisema lengo la kuundwa kwa baraza hilo ni kuhakikisha mkakati wa CCM kujiimarisha kiuchumi na kujitegemea katika shughuli zake unafanikiwa.

Alisema bazara hilo ni la kwanza kuundwa baada ya marekebisho ya Katiba ya CCM na kwamba litakuwa na jukumu la kusimamia mali za chama na jumuiya zake tatu yaani Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Umoja wa Wazazi na Umoja wa Vijana (UVCCM).

“Ni Baraza ambalo limepewa jukumu la kutekeleza mapendekezo ambayo yametokana na ripoti za tume ya uhakiki wa mali za chama ambayo nilikuwa Mwenyekiti wake.

“Ni chombo muhimu ndio maana umeona Mwenyekiti amekutana nao na tumewapa taarifa ya awali kuhusu kazi zao na nyenzo zikiwamo kanuni za fedha za chama  na katiba ya chama,” alisema Bashiru.

Alisema chama hicho kina lengo la kuhakikisha rasilimali na mali za chama hicho vinatumika kuboresha masilahi ya watumishi kuhakikisha wanakuwa na kipato cha uhakika wakati wa uchaguzi.

Alisema katika ripoti ya awali ambayo ilikabidhiwa kwa Mwenyekiti, Dk. Magufuli, kulikuwa na mapendekezo mengi ikiwamo kuhakikisha madeni ya chama yanahakikiwa.

“Mengine ni kuhakikisha mali za chama zinasajiliwa, nyaraka na mali za chama zinatunzwa, mali zilizoibiwa zinarejeshwa, kesi zilizoko mahakamani zinashughulikiwa na mambo kama hayo.

“Kama kuna mikataba ambayo ina matatizo inarekebishwa, kwa hiyo ni baraza la kwanza kupewa jukumu kubwa la ripoti hiyo,” alisema Dk. Bashiru.

Alisema baraza hilo pia litasimamia uhakiki wa mali kwa upande wa Zanzibar kwa kuwa ripoti iliyopo ni ile ya Tanzania Bara pekee.

“Ile ripoti iliyopo sasa, tume ilifanya kazi kubwa kwa upande wa Tanzania Bara, upande wa Zanzibar nadhani kwa mwezi huu au ujao inabidi tuanze kutuma kamati tuweze kuhakiki mali za Zanzibar ili kuwe na taarifa ya kutosheleza kuonesha mali za chama upande wa Zanzibar na upande wa Tanzania Bara,” alisema Dk. Bashiru.

Inaendelea………………. Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles